MAJI LAMU

Uhaba maji huko Manda kaunti ya Lamu huenda ukapungua baada ya serikali kuzindua miradi ya kukusanya maji ya mvua kwa kutumia matangi.

Uzinduzi huo umefanywa mapema leo na waziri wa maji Simon Chelugui katika shule ya upili ya Bin Fadhil na shule ya upili ya Wuyoni.

Miradi hiyo inajumuisha matangi ya maji ya chini ya ardhi yenye uwezo wa kuhifadhi lita laki moja za maji zitakazowafaidi wakaazi elfu moja katika kila shule.

Akihutubu wakati wa uzinduzi huo waziri Chelugui amewataka wenyeji kuitunza miradi hiyo.

Miradi mingine 10 zaidi itatekelezwa katika shule za eneo hilo.

Total Views: 85 ,