Mahakamani Kilifi

Mahakaman moja  mjini Kilifi imeamrisha kuhamishwa kwa mtoto wa darasa la sita  anayekabiliwa na shtaka la kujaribi kuavya mimba kutoka kwa jela baridi ya shimo la tewa hadi ile ya watoto ya mjini Malindi.

Kulingana na Hakimu Mwandamizi Dominica Nyambu, msichana huyo aliyezaliwa tarehe 29 agosti mwaka wa 1998 bado hajafikia miaka kumi na nane hivyo basi ni kinyume cha sheria kumzuilia katika  rumande ya shimo la tewa.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 14 mwezi wa saba mwaka huu.

Mwisho

Total Views: 405 ,