Mahakama Yaagiza Mwanahabari Jacque Maribe na Mpenziwe Wafanyiwe Uchunguzi wa Akili

Mahakama kuu mapema leo imeagiza kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kwa mwanahabari Jacque Maribe  sawia na matibabu kwa mpenziwe Joseph Irungu alias Jowie, kabla ya kuitikia mashtaka ya mauaji dhidi yao.

Jaji wa mahakama kuu Jessie Lesiit  pia ameagiza Maribe kuziliwa  katika gereza la wanawake Lang’ata huku Jowie akizuiliwa  katika gereza Industrial Area  hadi siku ya jumatatu ambapo watafikishwa mahakamani.

Wakili wa Jowie  Cliff Ombeta amelalamikia mahakama kuwa mteja wake hakuwa amepata matibabu kutokana na jeraha la risasi katika tukio la kujaribu kujitoa uhai licha ya agizo la mahakama ya Kiambu kutaka apate matibabu majuma mawili yaliyopita alipowasilishwa mbele yake.

Total Views: 162 ,