Magavana wakongamana Kakamega

Kongamano la tano kuhusu ugatuzi limeng’oa nanga katika kaunti ya Kakamega ambapo serikali inapania kutathmini mfumo huo mpya wa uongozi miaka mitano baada ya kuanza kutekelezwa nchini.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kufungua rasmi kongamano hilo kesho ambapo miongoni mwa maswala atakayoyazungumzia kwenye kikao hicho ni utekelezaji wa agenda zake nne muhimu katika kipindi chake cha mwisho uongozini.

Zaidi ya washiriki elfu sita wakiwemo magavana,manaibu wao,wanachama wa mabunge ya kaunti miongoni mwa wengine wanashiriki kongamano hilo la siku nne huku ikibainika kuwa idadi hiyo imezidi idadi ya vifaa vya malazi katika kaunti hiyo na pia kaunti jirani.

Wengine wanaotarajiwa kuhutubia kongamano hilo ni naibu wa rais William Ruto, kinara wa chama cha ODM Raila Odinga,kiongozi wa wachache katika seneti James Orengo miongoni mwa wengine.

Mwisho

Total Views: 241 ,