MAGAVANA NA KAUNTI

Mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya, amehimiza mawaziri wa fedha kwenye kaunti zote 47 humu nchini kushughulikia malipo ambayo hayajalipwa katika kipindi kilichopita cha matumizi ya fedha kufikia leo jioni.

Kwenye taarifa kwa wanahabari, Oparanya alihimiza mawaziri wote 47 kushughulikia haraka jambo hilo ili kuufungua mwaka mpya wa matumizi ya fedha bila deni.

Alisema kufuatia usambazaji fedha kwa serikali za kaunti na serikali ya kitaifa, amekubaliana na waziri wa fedha Henry Rotich kuruhusu serikali za kaunti kuendesha shughuli za kifedha hadi leo, kuhusiana na malipo yote ambayo hayajalipwa.

picha hisani

 

Total Views: 17 ,