Madkatari Tawain wapata Nyuki kwenye jicho la Mwanamke

Madktari  huko Taiwn wamepata nyuki wanee katika jicho la mwanamke mmoja aliyekwenda kutafuta matibabu kutokana na jicho lake kufura.

Hung Chi-ting daktari mkuu wa idara ya matababu ya macho katika hospital ya chuo kikuu cha  Fooyin  asema aligundua miguu ya wadudu hao yakiwa chini ya jicho lake la kushuto. Kisha baadaye aliwaona vizuri alipowatazama kwa kifaa cha microscope na kugundua kuwa wanne hao walikuwa hai.

Daktari Hung Chi-ting asema nyuki hao walitoboa kuwa hai kwa kuwa walikuwa wanatumia machozi ya mwanamke huyo  kama chakula.

Baadaye nyuki hao waliondolewa na mwanamke huyo kutibiwa athari walizokuwa wamesababisha .

Daktari wa hospitali hiyo wanasema hayuko katika hali ya hatari na atapata nafuu hivi karibuni

Total Views: 25 ,