Madaktari warejea kazini

Hatimaye Mgomo wa madaktari uliodumu kwa siku mia moja umefikia mwisho hivi leo na madaktari wanatakiwa kurejea kazini kuanzia kesho.

Mgomo huo umesitishwa baada ya wizara ya afya ,baraza la magavana na maafisa wa muungano wa madaktari kutia sahihi mpango wa pamoja wa kurejea kazini uliofikisha kikomo mgomo huouliosababisha machungu kwa wakenya.

Makubaliano hayo yalitiwa sahihi dakika chache kufikia mwendo wa saa kumi na mbili jioni ya leo katika jumba la dekta jijini Nairobi.

Mwisho

Total Views: 264 ,