Madaktari wa Cuba tayari kuwasili nchini

Sasa ni rasmi kuwa madaktari walio wataalam kutoka nchini CUBA watawasili humu nchini baada ya serikali kutia sahihi makubaliano rasmi kuhusu mpango huo.

Waziri wa Afya aliye nchini Cuba Sicily Kariuki amesema kuwa sehemu ya makubaliano hayo yaliyotiwa sahihi yatafanikisha mpango wa kupewa mafunzo kwa jumla ya madaktari hamisni kutoka humu nchini,nchini Cuba.

Mpango huu uliafikiwa kufuatia ziara ya rais nchini Cuba mwanzoni mwa mwezi huu ambapo ni miongoni mwa mikakati ya serikali katika kufanikisha agenda zake kuu nne ikiwemo huduma za matibabu kwa bei nafuu kwa wananchi.

Haya yanajiri huku madaktari wa humu nchini wakitofautiana na mpango huo wakidai kuwa hawakuhusishwa kabla ya maafikiano hayo ambapo wanasema unakinzana na shinikizo zao za kutaka kuajiriwa kwa madaktari waliohitimu na ambao hawajaajiriwa.

Mwisho

Total Views: 202 ,