Mabadiliko katika idara ya polisi, Mombasa yapata Kamanda mpya

Kaunti kadha nchini ikiwemo Garissa,Taita Taveta,Tharaka Nithi,Kajiado na hapa Mombasa zina makamanda wapya wa polisi.

Kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kutoka kwa ofisi ya naibu inspekta wa polisi Joel Kitili , jumla ya makamanda watano wapya wameteuliwa sawia na kuwapa uhamisho jumla ya maafisa 59 wakuu wa polisi kuhudumu maeneo mbali mbali ya nchi.

Paterson Maelo sasa ndiye kamanda mpya wa polisi hapa Mombasa huku Manse Musyoka akiteuliwa kuhudumu katika kaunti ya  Garissa ambapo wawili hao wameteuliwa ili kusaidia kukabiliana na visa vya utovu wa usalama vinavyoshuhudiwa.

Aliyekuwa hatibu wa polisi Zipporah Mboroki kwa sasa ni OCPD wa Lari huku Rop Kipkemboi akiteuliwa kuwa kamanda wa polisi katika kaunti ya Taita Taveta huku Julius Wanjohi akisalia kuwa kamanda wa polisi wa eneo la Pwani.

Mwisho

Total Views: 456 ,