Maafisa Waliompiga Risasi Mwanafunzi Wachukuliwa Hatua za Kisheria

Mbunge wa Kaloleni Paul Katana anasema kuachishwa kazi kwa maafisa wanaodaiwa kumuua mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Ndatani mwishoni mwa mwezi Juni  hakutoshi bali wanatakiwa kufunguliwa mashtaka.

Kwenye mahojiano ya kipekee na Pwani FM Katana anasema anaendelea kukusanya ushahidi  kwa kuwa maafisa hao wa polisi wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kudhihirisha kuwa kijana huyo alikuwa jambazi.

Katana Kazungu Fondo mwenye umri wa miaka 17 alipigwa risasi alipokuwa anasaidia lori lilokwama kwenye matope  na wenzake watano huku mbunge huyu akifichua kuwa kuna habari za kutatanishwa zilizotolewa kwa maafisa wa polisi.

Total Views: 139 ,