Lusaka ndiye spika wa Seneti

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Bungoma Ken Lusaka amechaguliwa kuwa spika wa bunge la Seneti baada ya kujizolea jumla ya kura 42 dhidi ya mshindani wake wa karibu Farah Malim aliyepata kura 25.

Afisa rejeshi aliyesimamia uchaguzi huo aliye pia karani wa bunge hilo Jeremiah Nyegenye ,alimtangaza Keneth Magelo Lusaka kama spika wa pili wa bunge hilo kwenye uchaguzi huo ulioingia duru ya pili.

Kwenye duru ya kwanza Ken Lusaka alipata kura 40,Farah Maalim 23 na Ekwe Ethuro kura mbili na kulazimisha duru ya pili kwani hakuna aliyepata thuluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kutangazwa mshindi kwa mujibu wa sheria za bunge.

Mwisho

Total Views: 215 ,