Ligi ya SportPesa kurudi Tena

Ligi kuu ya kitaifa humu nchini itarudi tena juma lijalo siku ya jumatano kwa mechi mbili baada ya mapumziko ya kimataifa.

Ulinzi stars watakuwa wanavaana na klabu ya Ingwee ambapo wote wamo katika nafasi ya 6 na 12 mtawalia katika jedwali la ligi kuu ya kitaifa.

Wanamvinyo Tusker Fc ambao wanaongoza ligi wakiwa na alama 48 watakuwa ugenini katika uga wa Mabaraki kuchuana na wawakilishi wa Pwani Bandari Fc ambao wanashikilia nafasi ya 11 wakiwa na alama 29.

Total Views: 354 ,