Laki moja kwa yule atakayebwaga simu yake ya Smartphone kwa wiki Moja.

Bila shaka utakubaliana nami kuwa wengi wetu kwa sasa tumezoea simu za touch screen kutokana na kuitimia kwa mambo mengi ikiwemo mitandao ya kijamii.

Na sasa kampuni moja katika jimbo la Utah huko Marekani imetoa jumla ya dola elfu moja sawa na shilingi laki moja za Kenya kwa Yule atakayewacha kutumia simu yake ya smart kwa wiki moja na badala yake kutumia simu ya kawaida tu.

Na si mtu yeyote tu anaweza kujitoza katika shindano hili. Wanatufata watu walio na uraibu wa kutumia smart phones, watalaamu wa mitandao ya kijamii na wale waliobobea pia kitechnolojia.

Total Views: 39 ,