Kylie Jenner Abarikiwa na Binti

Nyota nchini Marekani Kylie Jenner bado hajaamua atamupa jina gani bintiye  aliyebarikiwa siku ya Jumpaili .

Kylie mwenye umri wa miaka 20 aliwaweka wafuasi wake gizani kuhusiana na uja uzito wake.

Na hitimaye kwenye mtandao wake wa Instagram alisema kuwa alibarikiwa na binti February Mosi na bado wanatafakari watampa jina gani.

Mtoto huyo ni wa kwanza wa Jenner na mpenzi wake Travis Scott ambaye ni rapa mashuhuri Marekani.

Kylie Jenner, ambaye ni mtoto wa mwisho katika familia ya Kardashian na Jenner, alibobea kupitia kipindi cha televisheni ‘Keeping Up with the Kardashians’, pamoja na dada zake Kendall Jenner, Kourtney, Kim, na Khloé Kardashian.

Yeye ni binti wa mwanariadha wa olimpiki Caitlyn Jenner na nyota mashuhuri wa Televisheni Kris Jenner.

Total Views: 247 ,