Kuria Apongeza Kuteuliwa kwa Matiangi’

Mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria amepongeza hatua ya rais Uhuru Kenyatta kumteua waziri wa usalama wa taifa Fred Matiang’i kuwa msimamizi wa miradi ya serikali.

Kuria ameitaja hatua hiyo kuwa miongoni mwa mabadiliko kabla ya kura ya maoni akisisitiza kuwa Matiangi’ atasawasaidia Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto katika kuliongoza taifa ipasavyo.

Kauli yake inajiri siku moja baada ya rais Uhuru kumteua waziri Matiang’i katika wadhfa huo wakati wa kikao cha kufahamishwa makamanda wapya wa polisi katika maeneo mbali mbali nchini

Total Views: 83 ,