Kupigwa marufuku kwa kiboko kwalaumiwa

 

Kupigwa  marufuku kwa adhabu ya kiboko katika shule za umma kote nchini, kumetajwa kuathiri pakubwa sekta ya elimu  na kusababisha utovu wa nidhamu miongoni mwa  wanafunzi.

Haya yaliibuka kwenye kongamano la walimu wakuu wa shule za upili  ,sawa na washika dau mbalimbali katika sekta ya elimu wakiongozwa na  kamishna wa kaunti hiyo Josphine Onunga.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kongamano hilo lilofanyika mjini voi, kamishna huyo amesistiza haja ya kutumia mbinu  mbadala za  adhabu  kuwarekebisha wanafunzi watundu shuleni.

Hata hivyo amewataka wazazi sawa na jamii kwa jumla katika kaunti hiyo kudumisha maadili mema katika kaunti hiyo ya Taita-Taveta ili kukuza uongozi bora katika siku za usoni.

Kongamano hilo lililenga kutathimini na kutafuta suluhu dhidi ya  uchomaji wa shule katika kaunti hiyo baada ya njama ya kuchomwa kwa shule ya upili  ya wavulana ya  voi na kitobo  kutibuliwa juma lililopita.

Total Views: 429 ,