Kundi la kwanza la kikosi cha olimpiki kuelekea Rio wiki ijayo

Kundi la kwanza la timu ya Kenya itakayoshiriki katika mashindano ya olimpiki litaondoka nchini juma lijalo likiandamana na baadhi ya maafisa kuelekea nchini Brazil juma lijalo.

Kamati ya kitaifa ya olimpiki chini ya uongozi wake Stephen Arap Soi tayari imetoa ratiba ya usafiri kwa kikosi ambacho kitaondoka nchini mnamo tarehe 24 juma lijalo kuelekea Brazil.

Soi ameyasema haya baada ya kufungua rasmi kambi ya mazoezi ya timu ya Kenya iliyofunguliwa rasmi na waziri wa michezo Daktari Hassan Wario katika eneo la Eldoret.

Total Views: 370 ,