KUMBUKUMBU TAITA

Mataifa zaidi ya 10 yanatarajiwa kushirikiana na Kenya katika maadhimisho ya miaka 100 tangu kukamilika kwa vita vya kwanza vya dunia kaunti ya Taita Taveta yatakayofanyika kati ya tarehe 23-25 mwezi Novemba mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake meneja mkuu wa hoteli ya Sarova Taita Hills Willy Mwadilo amesema kuwa maadhimisho hayo yataleta pamoja mataifa yaliyoshiriki katika vita hivyo kati ya mwaka 1914-1918.

Insert Willy….

Mwadilo ameongeza kuwa ujio wa mataifa hayo kutaongeza uwekezaji na kufanya kaunti hiyo kuwa kitega uchumi katika sekta ya utalii huku akihimiza ushirikiano kati ya wananchi wa humu nchini na wale wa kigeni.

Insert Mwadilo….

Kaunti ya Taita Taveta ilikuwa moja ya ngome za kivita huku baadhi ya silaha zilizotumika zikihifadhiwa katika makavazi madogo ya hoteli ya Sarova Taita hills sawia na utunzi wa makaburi ya waliofariki katika vita hivyo na hutumika kama kivutio kwa watalii.

Total Views: 183 ,