Kula matunda na mboga kunaweza kukuongezea maisha

Watafiti sasa wanapendekeza kuwa kula matunda na mboga mara 10 kwa siku huenda kukusaidia kuishi kwa muda mrefu.

Utafiti huo umefanywa na chuo cha Imperial huko London na kubaini kuwa hali hiyo inaweza kupunguza vifo  milioni 7.8  kila mwaka.

Watafiti hao wametaja mboga kama vile spinach kudhibiti  saratani na matunda kama apples, pears na ndimu kudhibiti maradhi ya moyo.

Dkt Alison Tedston mkuu wa lishe bora huko uingereza asema  bado hawajafahamu iwapo kula matunda na mboga kwa pamoja huenda ukawa na manufaa tele ya afya.

Total Views: 243 ,