Kongamano la Shule za Upili lang’oa nanga Jijini Mombasa

Kongamano la 44 la kila mwaka la muungano wa walimu wakuu wa shule za upili, KESSHA limengoa nanga leo hapa Mombasa ambapo mkurugenzi wa tume ya huduma za walimu, TSC Reuben Nthamburi atalifungua rasmi.

Masuala ibuka wakati wa kongamano hilo linalohudhuriwa na zaidi ya walimu elfu 8 ni kufuatia kampeni iliyolenga wanafunzi elfu mia moja thelathini ambao walimaliza darasa la nane mwaka uliopita na hawakuwa wamejiunga na kidato cha kwanza pia yanatarajiwa kujadiliwa kwenye kongamano hilo.

Mwenyekiti wa Muungano huo Indimuli Kahi amesema kwamba kwenye mjadala huo mapendekezo kuhusu changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikishuhudiwa kwenye shule za upili kufuatia asilimia kubwa ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka huu yataangaziwa.

Aidha suala la utekelezaji wa Mtalaa wa Umilisi, CBC linatarajiwa kujadiliwa kwa kina.

Kongamano hilo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na waziri wa elimu, Prof. George Magoha.

Total Views: 7 ,