KOLOSH KUTETEA KITI CHAKE KWA TIKETI YA JUBILEE

Chama cha Jubilee kwa kauli moja kimemteuwa Mohamed Ahmed Kolosh kuipeperusha bendera yake katika uchaguzi mdogo wa Wajir Magharibi utakaofanyika tarehe 25 mwezi Aprili.

Kolosh ndiye aliyekuwa mbunge wa eneo hilo na aligombea kiti hicho kwa tiketi ya chama cha ODM kabla kubatilishwa kwa ushindi wake na mahakama ya juu mnamo tarehe 18 Januari mwaka huu.

Akithibitisha hatua hiyo naibu rais William Ruto amesema kama chama watajizatiti kuhakikisha kuwa wamekinyakua kiti hicho.

Ruto amesema kuwa hawakushinda kiti cha Wajir Magharibi,kwenye uchaguzi mkuu wa aAgosti nane mwaka 2017 kwa kuwa chama cha Jubilee hakikuwa na mgombea.

Kubatilishwa kwa ushindi wa Kolosh kulitokana na kesi iliyowasilishwa mahakamani na mlalamishi Abdirahiman Ibrahim Mohamed.

Wakati huo huo naibu rais amesistiza kuwa mikakati zaidi inaendelezwa na serikali ili kuliboresha zaidi eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Wagombea wengine waliojibwaga ulingoni kwenye kinyang’anyiro hicho ni Ibrahim Sheikh wa chama cha Kanu na Yusuf Elmi wa chama cha ODM miongoni mwa wengineo.

Total Views: 69 ,