KNUT na KUPPET washtumu hatua ya SRC ya kukadiria mishahara

Miungano ya vyama vya walimu KNUT na KUPPET imekashifu shughuli ya utathmini wa utendakazi kuhusu walimu inayoendeshwa na tume ya kukadiria mishahara SRC na kuitaja kama kupoteza pesa na wakati.

Wakizungumza na wanahabari katibu wa KNUT tawi la Kilindini Dan Aloo na mwenzake wa KUPPET Lynette Kamadi wamesema kuwa walimu wanaotaka kuwatathmini tayari wanafahamu kazi yao.

Aidha vyama hivyo vimesistiza kulipwa kwa nyongeza ya mshahara ya asilimia 50 – 60 waliyokuwa wamekubaliana na mwajiri wao TSC, swala ambalo wamependekeza kujumuishwa kwenye bajeti ya mwaka la sivyo wachukue hatua kwa mujibu wa sheria.

Haya yamejiri kwenye mkutano uliowaleta pamoja walimu wakuu na manaibu wao hapa Mombasa ili kujadiliana kuhusu utendakazi wao ili kuipa nafasi SRC kuwatathmin

Total Views: 355 ,