Kiraithe Alamu Kaunti dhidi ya Kufanikisha CCTV

Msemaji wa serikali, Erick Kiraithe amezitaka serikali za kaunti kuwajibikia juhudi zao za kuhakikisha kila mwananchi katika maeneo yao wako salama.

Aidha amehoji kuwa wafanyikazi wa serikali nchini pamoja na serikali za kaunti ndio wanaopaswa kunyoshewa kidole cha lawama kwa utumizi mbaya wa kamera za CCTV kwa kukosekana kwa taa za barabarani ambazo ni kiungo muhimu katika kazi ya kamera hizo nyakati za usiku.

Kiraithe amesema Kaunti ya Mombasa ni moja wapo ya maeneo yanayotumiwa na wahalifu kujificha,  akiahidi kuwa serikali pamoja na polisi watafanya wawezavyo kuhakikisha wahalifu hao wamekamatwa.

Total Views: 78 ,