Kinondo Warudi debeni

Wapiga kura katika wadi ya kinondo  eneo bunge la Msambweni kaunti ya kwale wanaoshiriki uchaguzi mdogo wa wadi hiyo wanalalamikia  kwendeshwa pole pole kwa zoezi hilo licha ya wapiga kura hao kujitokeza mapema.

Wakizungumza na Meza yetu ya habari wametaka maafisa wa iebc eneo hilo kuhakikisha wapiga kura  wanapiga kura kwa wakati ufaao ili kushugulikia masuala mengine ya ujenzi wa taifa.

Wadi ya kinondo  ina jumla ya vituo 21 na wapiga kura  elfu 11 huku ushindani mkali ukitarajiwa kati ya Juma Maone wa Jubilee na  Hamisi Pweza wa ODM.

Wakaazi hao wamerudi debeni tena baada ya wagombea hao kupata kura sawa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti.

Total Views: 202 ,