Kindumbwe ndumbwe cha ngao ya Gotv

Mabingwa watetezi wa ngao ya GOtv Shield Bandari fc watapiga ngarambe yao ya kwanza kupambana klabu ya Tezo huku klabu ya Gor ikitoka sare na klabu ya mahakama katika kipute hicho.

Mabingwa wa ngao hiyo mwaka 2013 AFC leopards watapiga mechi yao ya kwanza dhidi ya Mumbi National ,wanamvinyo Tusker Fc wachuane na Machakos united,huku thika United, Muhoroni, Western Stima na Chemelil zikipimana nguvu na vilabu vya Vapour, Amani Youth, Limuru na Nyakach FC mtawalia.

Aidha.. Vilabu vitatu vinavyoshiriki katika ligi kuu ya soka ya Sportpesa havitashiriki katika mashindano ya mwaka huu ya kuwania ngao ya GOtv, huku shirikisho la soka humu nchini likithibitisha kuwapo kwa timu 64.

Kwa mara ya pili mfululizo, Mathare United haitashiriki kwenye mashindano hayo sawa na Nairobi City Stars na Sofapaka.
Aidha, timu za Sofapaka na Mathare hazitashiriki kwa sababu zinataka kuangazia michuano ya ligi kuu nayo City Stars haitashiriki kwa sababu kinara wake Peter Jabuya amesema shirikisho la soka humu nchini halikuwaelezea kuhusu mashindano hayo na taratibu za kujisajili.

Kinara wa Mathare United Jacktone Obure amesema kilabu chake kinataka kuangazia mechi za ligi kuu pekee. Mabingwa wa mwaka 2010 na 2014 Sofapaka wamejiondoa kwa sababu nao pia wanawania kufanya vyema katika mechi za ligi ya Sportpesa ili kujikwamua katika hatari ya kushushwa daraja msimu ujao. Mashindano hayo yataanza rasmi tarehe 25 mwezi huu.

Total Views: 432 ,