Kindiki kuwasilisha hoja ya kumuondoa waziri Kaimenyi afisin

 

Kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Kithure Kindiki amesisitiza kwamba atawasilisha hoja  ya kutaka kuondolewa afisini kwa  waziri wa ardhi Prof.Jacob Kaimenyi kwa kushindwa kutatua mzozo wa kimpaka wa Meru-Tharaka Nithi.

Akiongea katika kanisa la Ntutuni ,seneta huyo wa kaunti ya Tharaka Nithi amemkashifu Kaimenyi kwa madai  kuwa  ana kiburi na kwamba anaingiza siasa katika suala hilo.

Kindiki amesema hana kisasi binafsi na waziri huyo kwa kuwa ni mmoja wa watu waliomuidhinisha kama mrithi wa aliyekuwa waziri wa ardhi Charity Ngilu.

Amesema alikua na matarajio makubwa kwamba Kaimenyi angesuluhusisha mzozo huo wa kimpaka baina ya kaunti hizo mbili punde atakapoapishwa kuanza kutekeleza majukumu yake.

Kiongozi huyo anasema ni wazi kwamba waziri aliyeondoka Charity Ngilu alikuwa amejitolea kikamilifu kutatua mzozo huo licha ya kwamba si mwenyeji wa eneo hilo huku akipuzilia mbali madai ya Kaimenyi kwamba kamati imeundwa kushughulikia suala hilo akisema ni siasa duni.

Total Views: 343 ,