Kilio Cha Wakaazi wa Wundanyi Cha Maji

Wakaazi wa  wadi ya Werugha Mjini Wundanyi kaunti ya Taita Taveta wameitaka serikali ya kaunti hiyo kushughulikia changamoto ya uhaba wa maji  eneo hilo ili kuwaepushia dhiki hiyo.

Wakiongea wakati wa zoezi la kukusanya maoni ya bajeti  linaloendelea katika vituo mbali mbali mjini humo, wananchi hao wamesema licha ya eneo hilo kuwa na chemichemi za maji  bado uhaba wa bidhaa hiyo ungali changamoto kuu.

Kwa sasa wamependekeza serikali kuwajengea  visima vya maji vya kutosha wakati serikali inatafuat suluhu la kudumu dhidi ya swala hilo.

Kadhalika wameitaka wizara ya maji na usafi wa mazingira kubadilisha mifereji ya maji iliyopo kwa sasa kwani mingi ya mifreji hiyo imezeeka na huharibika mara kwa mara.

Total Views: 70 ,