Kilifi:Akina mama,walemavu na vijana wanufaika na hazina ya Mbegu fund

Makundi ya akina mama na vijana wajasiriamali kaunti ya Kilifi yamepigwa jeki baada ya kukabidhiwa jumla ya shilingi milioni 30,kupitia mradi wa hazina ya Mbegu Fund,ili waweze kujiendeleza katika miradi ya kibiashara na kilimo biashara.

Pesa hizo zimetolewa kama mkopo ambao hautatozwa riba.

Akizindua rasmi hazina hiyo mapema leo, gavana Amason Kingi amesema serikali yake imechukua hatua ya ufadhili huo baada ya kugundua kuwa wengi wa wakaazi wa Kilifi wamekuwa wakikumbwa na ukosefu wa mtaji.

Kingi amewahimiza walengwa kujizatiti ili mradi huo uwasaidie kujikimu mahitaji yao mengine.

Gavana huyo anasema serikali yake inanuia kuwasaidia wakaazi wote kutimiza ndoto zao za kimaendeleo.

Miongoni mwa makundi yaliyonufaika na fedha hizo ni pamoja;

-Dabaso tusaidiane women group lililopokea hundi ya shilingi-elfu 275

-Kilifi town disabled group likakabidhiwa hundi ya shilingi elfu 200

-Ule mwanzo women group lililopewa hundi ya shilingi elfu 100

-Kaloleni farmers co-op society wakapewa shilingi elfu 500

-Kibaokiche fish farmers

-Mariakani toilors

-Majajani focus physically impaired group

-Uwezo women group

Gavana Kingi amesema serikali yake itaiyasaidia kwa karibu makundi hayo na mengine ili kuhakikisha yameafikia malengo yake.

Wakati huo huo gavana pia amewapa changamoto akina mama kutoka Kilifi kuhakikisha wamewasilisha maombi ya zabuni kutoka serikali ya kaunti ili waweze kunufaika.

 

Total Views: 105 ,