Kijana wa miaka 11 akula Mara tano kwa Lengo la kumuokoa babake

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 11 huko Uchina  anakula mara tano kwa siku kwa lengo la kumuokoa babake.

Babake Luzikuan ana saratani ya damu na anapaswa kuongezewa damu maarufu kama bone marrow transplant.

Kijana huyo ndiye wa kipekee kwenye familia aliye na damu iliyoko kwenye kundi moja na babake.

Madaktari wanasema anapaswa kuwa na uzani wa angalau kilo 45 kuweza kumutolea babake damu.

Alipopimwa mara ya kwanza ana uzani wa kilo 30. Kwa sasa ameongeza takriban kilo 11.

Total Views: 25 ,