Kifaranga maajabu Malindi

Wakaazi wa kijiji cha Mkao Moto wadi ya Ganda kaunti ya Kilifi wameamkia kisa cha kushangaza baada ya kuku kuangua kifaranga mwenye miguu minne na mkia kama wanavyodai walioshuhudia.

Kwa mujibu wa Francis Tsuma mkaazi wa kijiji hicho,ni mara ya kwanza kwa kisa hicho kushuhudiwa miongoni mwa kuku ila si mara ya kwanza miongoni mwa mifugo kwani kuna mbuzi aliyezaa kiumbe kilichokuwa na sura inayofanana na mwanadamu.

Hata hivyo Kulingana na afisa wa mifugo katika kaunti ndogo ya Malindi,visa kama hivyo husababishwa na utumizi wa dawa kwa kuku wanaotaga sawia na hali ya mfugaji kutumia jogoo mmoja kwa mbegu kwa mda mrefu.

Kadhalka visa kama hivyo huibua mseto wa hisia miongoni mwa wakaazi huku wengine wakivihusisha na maswala ya itikadi wakidai kuwa huashiria hali fulani miongoni mwa jamii swala linalopingwa na wataalam wa mifugo.

Mwisho

Total Views: 355 ,