Kifafa Kinaweza Epukika

 

Shirika la afya duniani linabaini  kuwa maradhi ya kifafa yanaweza kudhibitiwa kwa asilimia 70 kwa kuweka mipango kabambe ya kuyazuia na kutibiwa.

Daktari Eddie Chengo mtaalamu wa kifafa anasema kuwa maradhi hayo yanasababishwa  na chochote kinachoweza kuumiza ubongo hasa kupitia ajali au wakati mtoto anapozaliwa.

Akizungumza na Pwani FM amewahimiza kina mama wajawazito kuenda katika kiliniki wakiwa wajawazito na pia kujufungulia hospitali ili kuwaepusha watoto kuumuzwa kina mama wapaojifungua.

Mtaalamu huyo amefichua kwamba kuna visa vingi vya waathiriwa wa maradhi hayo katika eneo la Pwani  kutokana na changamoto zinazoikumba.

Takwimu zinabaini kuwa takriban watu milioni moja wanakabiliwa na kifafa na kati ya kikundi cha watu 100 watu wawili wana kifafa.

Total Views: 211 ,