KERO LA TAKA JIJINI MOMBASA

Washikadau na mashirika ya mazingira kaunti ya Mombasa wameshirikiana kubuni mpango makhususi utakaokabiliana na tatizo la taka eneo hili kwenye harakati za kuboresha hadhi ya jiji hili.

Wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya Jomvu kuu ambaye pia ni mwenyekiti wa mazingira Athman Shebe almaarufu “Mukono” amesema kuwa swala la taka limekuwa changamoto kubwa katika kaunti ya Mombasa kwa mda mrefu hali inayopelekea hatua ya kuanzisha mikakati ya kufufua mtambo wa kusaga taka eneo la Jitoni.

Shebe aidha ameeleza kuwa desturi ya wakaazi kumwaga taka ovyo ndio imefanya mazingira kuwa mabaya akisema ni lazima tabia hiyo ikome mara moja na kuhakikisha kuwa taka hazikai siku nyingi katika majaa madogo yaliyopo.

Total Views: 70 ,