KENYA YAPIGA HATUA KATIKA KUPAMBANA NA UFISADI

Kenya imepunguza alama moja kwenye orodha ya  viwango vya ufisadi duniani.

Katika ripoti iliyotolewa na shirika la Transparency International Kenya ina alama 27 kati ya  100, ikilinganishwa na alama 28 ilizopata mwaka wa 2017.

Wakati huo huo Rwanda imeorodheshwa kuwa na kiwango cha chini sana cha ufisadi katika kanda ya Afrika Mashariki ikiwa na alama  56 na kufuatiwa na Tanzania kwa alama 36, ilhali  Burundi ina alama  17 .

Nchi zilizo na viwango vya chini sana vya ufisadi ni Denmark na  New Zealand ambazo zina alama  88 na 87, mtawalia .

Somalia, Syria na Sudan Kusini zina alama 10, 13 na 13 mtawalia kumaanisha ufisadi umekithiri.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Transparency International hapa nchini Samuel Kimeu ametaja ukosefu wa nia njema ya kisiasa hapa nchini kama  kizingiti kikubwa zaidi kinachokabili taasisi zilizopewa jukumu la  kupambana  na ufisadi

 

Total Views: 72 ,