Kenya Kuivaa Tonga , Raga ya Dunia

Timu ya taifa ya raga itaanza kampeni yake ya kombe la dunia dhidi ya Tonga, inayoorodheshwa katika nafasi ya 24 ulimwenguni katika uga wa AT&T jijini San Francisco, Marekani, mwendo wa satano usiku.

Baada ya kufuzu nusu fainali mara mbili mfululizo, mwaka 2009 jijini Dubai, na mwaka 2013 jijini Moscow, Urusi, Kenya itanuia kufuzu fainali ya mwaka huu jijini Francisco itakapotoana kijasho na Tonga katika mechi ya kuwania nafasi ya kushiriki kwenye raundi ya mchujo.

Aidha mshindi wa mchuano huo anatarajiwa kuchuana na Uscoti kwenye raundi ya mchujo, huku Uscoti ikiwa kati ya timu nane zilizopata ticketi ya moja kwa moja ya kushiriki raundi ya mchujo.

Mshambulizi bora wa Kenya, Collins Injera, pia anatarajiwa kuandikisha rekodi nyingine, huku akiwa mchezaji wa kwanza kushiriki katika mashindano hayo kwa mara ya tatu mfululizo.

Total Views: 160 ,