Kaunti ya Mombasa Inanuia Kufanya Mabadiliko ya Ada

Waziri wa ardhi nyumba na mipango wa  kaunti ya Mombasa Edward Nyale amewataka wamiliki wa raslimali mbali mbali kutembelea afisi zao  ili kuthibitisha ada zilizopendekezwa na idara hiyo kwa wamiliki hao.

Kwenye kikao na wanahabari Nyale anasema wizara hiyo inajizatiti kupata maafikiano ya ada ambazo hazitamlemea mwananchi  huku akitilia mkazo kuwa  kulingana na sheria, rasimu hiyo inapaswa kuchunguzwa upya kila baada ya miaka kumi..

Jopo huru litabuniwa ili kuchunguza mapendekezo ya ada hizo na kuiwasilisha katika bunge la kaunti kwa majadiliano ya kina.

Total Views: 165 ,