Kaunti kupokea mgao wake baada ya rais kutia sahihi mswada husika

Rais Uhuru Kenyatta leo katika ikulu ya Nairobi ametia sahihi mswada wa marekebisho kuhusu ugavi na mapato hatua inayoipa mamlaka hazina kuu ya serikali kusambaza pesa za mgao kwa serikali za kaunti.

Sheria hiyo mpya inaeleza bayana mgao maalum kwa serikali za kaunti ikiwemo mikopo na ruzuku hatua inayowianisha sheria hiyo ya mwaka wa 2017 dhidi ya sheria ya ugawaji wa pato la kitaifa ya mwaka wa 2017.

Rais Uhuru amesema kuwa ugawaji wa pesa hizo kwa sasa utaziwezesha serikali za kaunti kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya mwananchi

Waliokuwako wakati wa kutiwa sahihi kwa mswada huo ni naibu rais William Ruto,mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua,maspika Justin Muturi na Kenneth Lusaka,kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale na mwenzake wa Seneti Kipchumba Murkomen.

Mwisho

Total Views: 344 ,