Kasisi Akamatwa kwa Kumukosea Mfu.

 

Kasisi mmoja nchini Msumbiji amekamatwa na maafisa wa polisi kwa kile walichokitaja kumkosea mfu heshima.

Kasisi huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia asafiri hadi  hospitali ya Chimoio katika jimbo la Manica, kufanya muujiza huo.

Dada yake marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe anasema  kuwa kasisi  huyo aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha na kisha kumuzungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.

Na alijipata matatani hata pale hata sehemu  moja ya marehemu iliyoweza kutikisika licha hata ya kupasa sauti na kusema amka kijana wa Mungu.

Na hata baada ya siku mbili za maombi makali, hakuweza kabisa kurejesha uhai wa marehemu na maafisa wa polisi walimkamata kwa kusoa heshima mfu.

Total Views: 267 ,