Kariobangi wakaribia Kumnasa Odongo

Klabu ya Kariobangi Sharks inakaribia kukamilisha uhamisho wa mchezaji Cavin Odongo kutoka klabu ya Posta Rangers ili kuimarisha klabu hiyo ambayo kwa sasa imepandishwa daraja kusakata katika ligi kuu ya humu nchini.

Odongo amekuwa na mchango mkubwa katika klabu ya Posta Rangers ambapo alifunga mabao 4 na kusaidia klabu hiyo imalize katika nafasi ya nne msimu uliopita.

Total Views: 373 ,