Kaparo na bunge

Tume ya kitaifa ya maridhiano na mshikamano inapendekeza kubuniwa kwa sharia itakayowazuia wanaoeneza matamshi ya chuki kuwania nyadhifa za umma.

Mwenyekiti wa tume hiyo Francis Ole Kaparo aliyefika mbele ya kamati ya pamoja ya bunge kuhusu mshikamano pia aliwataka viongozi wa vyama vya kisiasa kuongoza juhudi za mshikamano kwenye makabiliano dhidi ya wanaoneneza matamshi ya chuki.

Kamati hiyo imeahidi kuhamisha shilingi bilioni 1 kutoka kwa wizara ya usalama wa taifa hadi kwa tume hiyo katika juhudi za kuimarisha mshikamano.

Mwisho

Total Views: 383 ,