Kaparo awataka wakenya kuwa na imani na Mahakama kuu

Mwenyekiti wa Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa Francis Ole Kaparo ametoa wito kwa wakenya kukubali matokeo ya uamuzi wa mahakama ya upeo kwenye rufaa ya kupinga uchaguzi wa urais inayoendelea kwa sasa.

Aidha Kaparo pia ameupongeza muungano wa NASA kwa kuchukua hatua ya kwenda mahakamani kwenye harakati ya kutafuta utatuzi dhidi ya lalama zao za kisiasa ikizingatiwa kuwa ndio njia mwafaka ya kikatiba.

Kadhalka amewataka wakenya kuendelea na shughuli zao za kawaida na kujitenga na wanasiasa na vyama vinavyoshinikiza taharuki wakati taifa linaposubiri uamuzi wa mahakama ya upeo.

Mwisho

Total Views: 225 ,