KANU yapinga matokeo

GEDION MOIChama cha KANU kimepinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa useneta katika kaunti ya Kericho ambapo mgombea wake Paul Sang alishindwa na mgombea wa JAP Aaron Cheruiyot.

Maafisa wa chama hicho na wafuasi wao wanadai kuwa uchaguzi huo haukuwa wazi na haki,huku wakiishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kwa madai ya kumpendelea mgombea wa JAP Aaron Cheruiyot.

Hata hivyo akiongea baada ya kupokea cheti chake cha ushindi katika uchaguzi huo mdogo,Cheruiyot amepuzilia mbali madai hayo huku viongozi hao wa KANU wakitishia kutoa matokeo yao kinyume kesho baada ya kudai kuwa maafisa wa usalama walishawishiwa.

Cheruiyot alishinda uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali kwa kujizolea jumla ya kura 109,358 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Paul Sang wa chama cha KANU aliyejizolea jumla ya kura 56,307.

Mwisho

Total Views: 374 ,