Kanisa na elimu

webukhalaKanisa la kianglikana nchini linaitaka serikali kushughulikia matatizo ibuka katika sekta ya elimu nchini ikiwemo mrundikano wa wanafunzi katika madarasa ,mishahara ya walimu na ukosefu wa hati miliki za ardhi kwa ardhi za shule.

Akizungumza wakati wa kongamano la shule zinazosimamiwa na kanisa hilo nchini,askofu mkuu Eliud Webukhala amesema kuwa kanisa linawajibika vilivyo kuhakikisha kuwa elimu inaboreshwa nchini kwa kujumuisha maadili.

Amedokeza kuwa kanisa liko tayari kushirikiana na serikali pamoja na washikadau katika sekta ya elimu katika kubuni mtaala mpya utakaohakikisha kuweko kwa elimu bora na mwafaka humu nchini.

Kadhalka amesema kuwa kwa sasa kanisa hilo limo mbioni kuhakikisha kuwa linapata hati miliki za ardhi ambazo zinafadhiliwa na kanisa la kianglikana nchini kwa manufaa ya uboreshaji wa elimu nchini.

Mwisho

Total Views: 400 ,