Kanisa lawataka wanasiasa kusitisha mzozano na kuangazia maendeleo

Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana nchini Jackson Ole Sapit ameutaka muungano wa NASA kusubiri uchaguzi mwengine wa urais mwaka wa 2022 ikizingatiwa kuwa rais Uhuru Kenyatta yuko ofisini kisheria.

Akizungumza na wanahabari,askofu Sapit amesema kuwa kipindi cha uchaguzi kilikamilika mwaka jana na kwamba ni wakati sasa kwa nchi kuwa na mazingira mwafaka ya maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi baada ya kubuniwa kwa serikali mpya.

Aidha ametoa wito kwa walio serekalini na wale wa upinzani kuanzisha majadiliano ya jinsi ya kuwaunganisha wakenya ambao ni dhahiri kuwa kwa sasa wamegawanyika kwa msingi wa kisiasa.

Mwisho

Total Views: 271 ,