Kampeni za Malindi zapamba moto.

Kampeini za uchaguzi mdogo wa ubunge katika eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi zinazidi kushika kasi huku gavana wa kaunti hiyo Amerson Jeffa Kingi akiwarai wapiga kura kumchagua mgombea wa kiti hicho kwa chama cha ODM Willy Mtengo.

Akiwahutubia wanachama wa mwavuli wa waendesha bodaboda katika kaunti ndogo ya Malindi,Kingi amesema simulizi la maendeleo kutoka kwa mrengo wa serikali halifai kutumiwa kama chombo cha kuendesha  kampeni kwani ni haki ya kila mmoja kwa sababu wanalipa ushuru.

Anasema ni makosa kwa muungano wa Jubilee kudai utaleta maendeleo katika eneo la Malindi iwapo wapiga kura watamchagua Philip Charo anayewania kiti hicho kupitia chama cha Jap,akisisitiza kwamba ni haki yao kupata maendeleo bila kujali chama cha kisiasa wanaochoegemea,.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mwavuli wa chama cha Waendesha bodaboda hao Joseph Mwangu amewataka wanasiasa kuunganisha wakenya wote sawa na kutoa wito kwa wanachama wenzake kufanya uamuzi wa sahihi wakati wa kuwachagua viongozi.

Total Views: 360 ,