JUHUDI DHIDI YA MIMBA ZA MAPEMA

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jeffa Kingi ametoa wito kwa viongozi wa kidini kuingilia kati makabiliano dhidi ya mimba za mapema kaunti hiyo.

Wito huo umetolewa huku kukiwa na taarifa kwamba idadi ya visa vya mimba za mapema miongoni mwa vijana inaendelea kuongezeka kutoka elfu 13 mwaka wa 2017 hadi visa elfu 17 mwaka wa 2018.

Akiongea mjini Kilifi, Kingi amesema wakati umewadia kwa kaunti hiyo kutafuta mwongozo wa kidini kukabiliana na mimba za mapema huku akiwalaumu wazazi kwa kushindwa kuzungumza na watoto wao kuhusu maswala ya afya ya uzazi.

Picha Hisani.

Total Views: 80 ,