Josephine Medza

Medza ni mchezaji wa mpira wa mikono anayesema wengi hawamini anaweza kucheza vyema japo kimo chake.

Anatambulika na wasikilizaji wake wa Kipindi cha Kimijikenda cha Dobedobeza anachokiendesha na mwenzake Gasper Tumaini kama msichana mjasiri anayekataa mila potovu za jamii hiyo.

Ungana naye, na mwenzake Gasper kila siku saa nane hadi saa kumi,wakustajibishe na visanga vinavyotendeka katika jamii ya Wamijikenda.

Medza anasema japo yeye si shabiki vile vile wa Kandanda lakini anafuatilia tu klabu ya Manchester United. Kila wakati anapopata mda, yeye hufanya hesabu na kushindwa kunamtia kiwewe.

Amesomea taluma ya uana habari kutoka chuo cha Technical University of Mombasa

Total Views: 3540 ,