JOHO ATETEWA

 

Mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa Mohammed Hatimy amewakosoa baadhi ya viongozi kutoka eneo la Bonde la Ufa na Mlima Kenya wanaodaiwa kumshambulia gavana Hassan Joho.

Hatimy amesistiza kuwa juhudi za wanasiasa hao hazitaishusha hadhi ya Joho kisiasa.

Mbunge huyo maalum katika serikali ya kaunti ya Mombasa,aidha anadai kuwa mfadhili wa wanasiasa hao anayedaiwa kuwa naibu rais William Ruto ameingiwa na tumbo joto kuhusu siasa za 2022.

Wakiongozwa na mwenyekiti Hamisi Dawa,wafanyibishara hao wamebainisha ghadabu zao kwa wanasiasa hao kwa kumhusisha Joho na  ulanguzi wa mihadarati.

Wafanyibishara hao wameyataja madai hayo kama tetesi zisizokuwa na msingi wowote,wakisema Joho ni mchapa kazi.

Waamewataka wanasiasa hao kukoma kuendeleza uvumi huo na badala yake wazingatie maendeleo katika maeneo yao.

 

Total Views: 83 ,