JOHO AJISAJILI RASMI

Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho amekuwa kiongozi wa hivi punde kusajiliwa kwenye mfumo wa kidijitali NIIMS maarufu Huduma Namba.

Akizungumza kabla ya kusajiliwa Joho ameonyesha kukerwa kwake kufuatia hatua ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakieneza propaganda kuhusu mfumo huo.

Kulingana na Joho mataifa mengi yameendelea kufuatia usajili sawa na huo ikizingatiwa kwamba unatoa fursa ya kuwezesha kuwapo kwa utoaji wa hudma bora zaidi kwa Wananchi hasa katika siku za usoni.

Joho amewahimiza wenyeji wa Mombasa kujitwika jukumu la kuhakikisha wanahamasishana ili watu wote wanaolengwa kusajiliwa kwenye mfumo huo ambao ni takriban milioni 1.5 kwenye kaunti hii wanasajiliwa.

Hayo yanajiri huku jumla ya makarani 411 wakiendeza shughuli ya kuwasajili watu kwenye maeneo mbalimbali ya Mombasa.

Akizungumzia masuala ya vita dhidi ya ufisadi na lile la kuwaunganisha wakenya ambayo yamekuwa yakiendelezwa na rais Uhuru Kenyatta, Joho amewakashifu vikali viongozi ambao wamekuwa wakirudisha nyuma juhudi hiyo.

Picha hisani.

Total Views: 24 ,