Jazi no. 7 yawekwa kabatini OldTrafford

Usimamizi wa klabu cha Manchester united umeweka bayana kuwa uliacha wazi jazi nambari 7 makusudi…msimu huu ili kuikabidhi kwa sajili bora zaidi itakayoweza kutinga mabao kwa klabu hicho..

Mourinho alishindwa kupata winga bora msimu huu baada ya Gareth Bale, na Ivan Periscic kukosa kutua ugani Old Trafford.

Taarifa zinasema kuwa United inatazamia kumsajili mchezaji Antoinne Griezmann kutoka Ufaransa anayewajibikia klabu cha athletic Madrid nchini Uhispania.

Griez angejiunga na United lakini akaamua kusalia klabuni humo baada ya Athletico Madrid kupigwa marufuku ya kusajili hadi mwezi januari..jazi hiyo iliwahi kuvaliwa na masogora George Best, Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckham ,Cristiano Ronaldo kabla ya kuvaliwa na Memphis Depay ambaye alikuwa na msimu mgumu kabla ya kueleka Olympique Lyonnais.

Total Views: 227 ,