ITUMBI AACHILIWA KWA MASHARTI

Afisa wa mawasiliano ya digitali katika afisi ya rais Dennis Itumbi ameachiliwa kwa dhamana ya shillingi laki moja pesa lakini kwa masharti ya kuripoti kwa kituo cha polisi cha Muthaiga kila siku isipokua wikendi.

Hii ni baada ya upande wa mashtaka kukosolewa kwa kushindwa kutoa ushahidi wa kutosha kufuatia madai waliyotoa awali kwamba huenda Itumbi angehitilafiana na uchunguzi iwapo mahakama ingemwachilia.

Hakimu Zainab Abdul pia aliukosoa upande wa mashtaka kwa kushindwa kutaja majina kamili ya waliohojiwa kutoka kwa kundi liliko kwenye mtandao wa Whatsapp la tangatanga.

Itumbi anatuhumiwa kuchapisha barua katika kikundi cha whatsapp cha mrengo wa Tangatanga, kundi ambalo linamuunga mkono Ruto kuwania urais mwaka 2022.

Ni madai ambayo Itumbi anayapinga akitaka kuruhusiwa kucheza video aliodai inaonyesha wapinzani wa Ruto wakiwa katika hoteli ya La Mada Nairobi wakipanga kumwangamiza Ruto, ombi ambalo halikukubalika mahakamani.

picha hisani

Total Views: 17 ,